
UTUMISHI
- Dodoma
- +255 734 986 508
- [email protected]
- Open Jobs – 1
Jukumu kubwa la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB) ni kuimarisha Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji na usimamizi wa shughuli za utumishi wa umma na kujenga uwezo wa watumishi wa Umma ili watoe huduma bora kwa wananchi. Kwa mujibu wa Hati ya Mgawanyo wa Majukumu kwa Mawaziri kama ilivyotangazwa katika Gazeti la Serikali Toleo Na. 619A&619B la tarehe 30/8/2023, OR-MUUUB ina majukumu yafuatayo:-
1.1 DIRA NA DHIMA
1.1.1 DIRA
Kuwa na “Utumishi wa umma wenye ufanisi na uwajibikaji katika kufikia ustawi wa Taifa"
1.1.2 DHIMA
“Kusimamia utumishi wa umma kupitia Sera, Mifumo na Miundo ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu iliyoboreshwa”
1.2 Maadili ya Msingi katika Taasisi
-Uzalendo
-Uadilifu
-Ubora
-Mteja Kwanza